
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amewasili kushiriki Hafla ya Kihistoria ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Kampasi ya Kagera ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).


