WAZIRI MKENDA AWATAKA VIJANA KUSIMAMIA KWA UWAZI NA UWADILIFU RASILIMALI ZA UMMA
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amewataka vijana nchini kuwajibika kikamilifu katika kusimamia matumizi sahihi ya rasilimali za umma, sambamba na kupinga vitendo vya rushwa.
TANZANIA NA IRELAND ZAIMARISHA USHIRIKIANO UFADHILI WA MASOMO YA JUU
Serikali ya Tanzania imeendelea kutoa ufadhili wa masomo katika elimu ya juu kupitia Samia Skilashipu, na mwaka huu imeanzisha Samia Scholarship Extended AI/DS

kwa ajili ya wanafunzi wa Shahada ya kwanza katika fani za data science, artificial intelligence, cyber security, machine learning na allied science
SERIKALI KURATIBU ASASI ZA KIRAIA ILI KUIMARISHA HUDUMA ZA ELIMU NA MATUMIZI YA RASILIMALI KWA UWIANO
Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetangaza kuanza kuratibu Asasi za Kiraia zinazotekeleza miradi ya elimu nchini, ili kupata taarifa sahihi kuhusu huduma wanazotoa na maeneo yanayonufaika, ili kuimarisha ushirikiano baina ya wadau wa elimu, kuongeza uwazi wa utekelezaji wa shughuli, na kuhakikisha kuwa rasilimali zinatumika kwa ufanisi zaidi katika maeneo yenye uhitaji mkubwa.
SERIKALI YAZINDUA MAFUNZO YA LMS NA DARASA JANJA KWA VIONGOZI WA ELIMU NCHINI
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI wameanza kutoa mafunzo ya Ufungamanishaji wa Mfumo wa Usimamizi wa Kujifunza (LMS) na Darasa Janja (Smart Class) kwa viongozi wa mikoa, halmashauri, kata na walimu nchini, yakiwa na lengo la kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji kwa njia ya kidigitali.

UTEKELEZAJI WA MRADI WA HEET UZINGATIE KUFIKIA MALENGO YA DIRA YA MAENDELEO YA TAIFA 2050 – PROF. NOMBO
Katibu Mkuu wa Wizarau ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, ametoa wito kwa wadau wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) kuhakikisha kuwa utekelezaji wa mradi huo unakuwa wa ubunifu, shirikishi, na wenye tija ili kuchangia kikamilifu katika kufanikisha malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, katika sekta ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA STASHAHADA YA UALIMU ELIMU YA AWALI NA MSINGI KWA MWAKA WA MASOMO 2025/2026 Awamu ya pili
TANZANIA NA QATAR KUENDELEZA USHIRIKIANO KUIMARISHA SEKTA YA ELIMU
Na
WyEST
Balozi wa Qatar Nchini Tanzania Mheshimiwa Fahad Rashid Al-Marekhi, leo tarehe 7 Agosti 2025, amekutana na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda katika Pfisi za Wizara Jijini Dar ES Salaam
Lengo kuu la ziara hiyo lilikuwa kujadili maeneo ya ushirikiano kati ya Tanzania na Qatar katika Sekta ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
TANZANIA NA INDIA KUENDELEZA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, leo Agosti 07, 2025 Jijini Dodoma amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Bishwadip Dey ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali ya Elimu na namna ya kuimarisha ushirikiano katika nyanja za sayansi na teknolojia.

