ORODHA YA WAOMBAJI WALIOCHAGULIWA KUPATA UFADHILI WA MASOMO KATIKA VYUO VIKUU BORA DUNIANI KATIKA FANI ZA SAYANSI YA DATA, AKILI UNDE, NA SAYANSI SHIRIKISHI KWA MWAKA 2025/2026
WAHITIMU 50 WAPATA UFADHILI WA SAMIA SCHOLARSHIP EXTENDED KUSOMEA AKILI UNDE NA SAYANSI YA DATA
WAHITIMU 50 WAPATA UFADHILI WA SAMIA SCHOLARSHIP EXTENDED KUSOMEA AKILI UNDE NA SAYANSI YA DATA
Wahitimu 50 waliofanya vizuri katika masomo ya Sayansi kwenye matokeo ya Kidato cha Sita mwaka 2025 wamechaguliwa kupata ufadhili wa Samia Scholarship Extended, kusomea programu za Akili Unde, Sayansi ya Data na Sayansi zingine Shirikishi katika vyuo vikuu mahiri duniani.
PROF. DANIEL MUSHI AMEFANYA ZIARA YA KIKAZI KATIKA TUME YA VYUO VIKUU (TCU)
Katika kuimarisha usimamizi wa elimu ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu nchini, Naibu Katibu Mkuu Prof. Daniel Mushi Agosti 29,2025 amefanya ziara ya kikazi katika Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) jijini Dar es Salaam.

Ziara hiyo ililenga kuweka Kwa pamoja mikakati ya kuendeleza elimu ya juu ili iwe ya ushindani wa kikanda na kimataifa.
SERIKALI KUIMARISHA ELIMU YA WATU WAZIMA: TEWW YAJIVUNIA MIAKA 50 YA MAFANIKIO
PROF MKENDA AKUTANA NA VIONGOZI WA TET NA KAMATI YA TUZO YA UANDISHI BUNIFU YA MWALIMU NYERERE
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Akutana na Viongozi wa TET na Kamati ya Tuzo ya Uandishi Bunifu ya Mwalimu Nyerere

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amekutana na kufanya mazungumzo na Baraza la Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) linaloongozwa na Mwenyekiti wake, Prof. Maulid Mwatawala, kujadili uendeshaji wa masuala mbalimbali ya taasisi hiyo.
SERIKALI KUIMARISHA ELIMU YA WATU WAZIMA; TEWW YAJIVUNIA MIAKA 50 YA MAFANIKIO
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa Serikali itaendelea kuiboresha Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) ili kuwezesha Watanzania walio nje ya mfumo rasmi wa elimu kupata fursa ya kujifunza na kuongeza ujuzi.
WAZIRI MKUU AITAKA WIZARA YA ELIMU KUONGEZA WIGO WA UPATIKANAJI WA ELIMU YA WATU WAZIMA
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, ameitaka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuendelea kupanua wigo wa upatikanaji wa Elimu ya Watu Wazima nchini.
PROF MKENDA TAASISI YA ELIMU YA WATU WAZIMA INATEKELEZA MAJUKUMU MENGI KWA MAENDELEO YA TAIFA
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amesema kuwa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima imepanua majukumu yake na sasa inatekeleza kazi kubwa zaidi ya suala la watu wazima kujua kusoma, kuandika na kuhesabu.
Akizungumza Agosti 25, 2025 jijini Dar es Salaam, Prof. Mkenda ameeleza kuwa taasisi hiyo imekuwa chachu ya mabadiliko katika elimu jumuishi na elimu bila ukomo kwa watu wote nchini.

