PROF. NOMBO: KONGAMANO LA MIAKA 50 NI FURSA YA TATHMINI NA MWELEKEO WA ELIMU YA WATU WAZIMA

Prof. Carolyne Nombo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, amesema kuwa Kongamano la Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 50 ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima limeandaliwa kwa lengo la kufanya tathmini ya mafanikio, changamoto na mwelekeo wa baadaye wa elimu ya watu wazima nchini.

Swahili

VIONGOZI WA WIZARA WATUNUKIWA KWA KULETA MABADILIKO CHANYA KATIKA ELIMU JUMUISHI

Viongozi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda na Katibu Mkuu Prof. Carolyne Nombo, wamepokea tuzo maalum kutoka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima zilizotolewa kama ishara ya kutambua mchango wao mkubwa katika kusimamia na kuendeleza Elimu ya Watu Wazima nchini, hususan kwa juhudi zao za kuimarisha sera, mipango na utekelezaji wa programu zinazolenga kuwajengea uwezo wananchi wa rika mbalimbali.

Swahili

PROF. NOMBO AKAGUA MAANDALIZI YA KONGAMANO LA MIAKA 50 YA ELIMU YA WATU WAZIMA

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amekagua maandalizi ya Kongamano la Maadhimisho ya Miaka 50 ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima linalofanyika leo Agosti 25, 2025 JNICC jijini Dar es Salaam.



Kongamano hilo linalenga kutathimini mafanikio ya Taasisi hiyo katika kuendeleza elimu jumuishi na endelevu kwa watu wazima nchini.

Swahili

WADAU MBALIMBALI WA ELIMU WAMESHIRIKI KATIKA KONGAMANO LA MIAKA 50 YA TAASISI YA ELIMU YA WATU WAZIMA

Wadau mbalimbali wa Elimu leo Agosti 25, 2025 jijini Dar es Salaam wameshiriki katika Kongamano la Miaka 50 ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kusherekea mafanikio ya taasisi hiyo tangu kuanzishwa kwake.



Kongamano hilo linahususha maonesho ya bidhaa za wanakisomo wa Taasisi hiyo zilizotokana na mafunzo ya vitendo na ubunifu wa washiriki.

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS