BOOST YAWEZESHA UTEKELEZAJI WA SERA YA ELIMU HALMASHAURI YA MERU
DKT. OMAR AITAKA TEWW KUVUKA MIPAKA KUWAFIKIA WASIOFIKIWA KIMASOMO
MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA TAASISI YA ELIMU YA WATU WAZIMA YAZINDULIWA RASMI
Prof. Adolf Mkenda ashiriki NBC Dodoma Marathon 2025
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, hii leo Julai 27, 2025, jijini Dodoma, ameshiriki NBC Dodoma Marathon kwa mwaka 2025 akikata upeo kilomita tano.

Marathon hiyo imehudhuriwa na watu wa rika mbalimbali na ilihusisha mbio za makundi tofauti ambapo Mgeni rasmi katika tukio hilo alikuwa ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Mashaka Biteko
MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA TAASISI YA ELIMU YA WATU WAZIMA YAZINDULIWA RASMI
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetangaza rasmi kuanza kwa wiki tatu za maadhimisho ya miaka 50 ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), yakilenga kuongeza uelewa wa jamii kuhusu umuhimu wa elimu nje ya mfumo rasmi. Kauli mbiu ya maadhimisho ikiwa ni “Elimu bila ukomo kwa maendeleo endelevu.”
ZAIDI YA WALIMU 900 WAPATIWA MAFUNZO YA TEHAMA
Mkoani Morogoro walimu 970 wamepatiwa mafunzo kupitia mradi wa SEQUIP.
Akihitimisha mafunzo hayo Julai 27, Naibu katibu Mkuu wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia anayeshughulikia masuala ya elimu Dkt. Hussein Omary akawasisitiza walimu kuhusu matumizi ya TEHAMA ili kuwezesha ambayo kuwafikia wanafunzi wengi hususani wanafunzi katika maeneo yote nchini.

