TANZANIA YAONGEZA KASI YA MAANDALIZI YA WATAALAMU WA NYUKLIA

Katika kuhakikisha usalama na uendelevu wa matumizi ya teknolojia ya nyuklia, Tanzania imeanza kuandaa rasilimali watu wa Sayansi na Teknolojia ya Nyuklia katika vyuo vya ndani na nje ya nchi Ili kujenga uwezo wa kitaifa na kupunguza utegemezi wa wataalamu kutoka nje ya nchi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, ameeleza hayo Vienna, Austria 17 Septemba 2025 wakati wa kikao maalum na Mkurugenzi wa Divisheni ya Afrika wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA), Dkt. Gashaw Gebeyehu Wolde, kando ya Mkutano Mkuu wa 69 wa IAEA.

Swahili

UTAWALA BORA KATIKA ELIMU CHACHE YA MAENDELEO YA ELIMU NJE MFUMO RASMI - MWL. HINJU OR - TAMISEMI

Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu ya Watu Wazima, Ofisi ya Rais–TAMISEMI, Mwalimu Ernest Hinju amesema kuwa uwajibikaji, uadilifu na uzalendo ni nyenzo muhimu katika maendeleo ya Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi.

Mwalimu Hinju amesema hayo Septemba 16, 2025 mkoani Katavi akiwasilisha mada kuhusu Muundo wa Uongozi bora kwenye Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi.

Swahili

PROF. NOMBO AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA IAEA VIENNA

Leo tarehe 15 Septemba, 2025, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Ignatius Nombo ameongoza Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano Mkuu wa 69 wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki unaofanyika katika Jiji la Vienna, Nchini Austria. Kulia kwa Katibu Mkuu ni Balozi wa Tanzania na Mwakilishi wa kudumu Nchini Austria, Mhe. Naimi S. H. Aziz

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS