Prof. Nombo amekutana Kiongozi wa Kampuni ya Empower Limited Miranda Naiman kujadili juu ya utekelezaji wa mitaala mipya

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amekutana Kiongozi wa Kampuni ya Empower Limited Miranda Naiman na kujadili juu ya utekelezaji wa mitaala mipya na mipango na mikakati ya kuboresha elimu ya juu nchini.

Swahili

Prof. Adolf Mkenda akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari juu ya Sera ya Elimu na Mafunzo

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari juu ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023 na Mitaala mipya ya Elimu ya awali msingi sekondari na Ualimu.



Prof. Mkenda amewaeleza Wahariri wao kuwa serikali imeanza kutekeleza Sera na Mitaala hiyo kwa baadhi ya ngazi za elimu huku akisisitiza kuwa utekelezaji huo unafanywa kidogo kidogo ili kuhakikisha unakuwa na mafanikio.

Swahili

Wahariri wa Vyombo vya Habari walipitishwa katika utekelezaji wa Mitaala iliyoboreshwa ya Mwaka 2023 ili wawe na uelewa wa maboresho hayo

Wahariri wa Vyombo vya Habari walipitishwa katika utekelezaji wa Mitaala iliyoboreshwa ya Mwaka 2023 ili wawe na uelewa wa maboresho hayo



Wahariri walipitishwa katika utekelezaji huo Mechi 07, 2024 Jijini Dar ea Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu (TET) Dkt. Anneth Komba wakati wa Mkutano wao na Viongozi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia uliolenga kuzungumza na kujadili juu ya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu.

Swahili

Serikali ya Awamu ya Sita imeweka kipaumbele katika Sekta ya Elimu hasa katika Ujenzi wa Miundombinu na kutoa Mafunzo Kwa Walimu kazini

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Carolyne Nombo amesema serikali ya Awamu ya Sita imeweka kipaumbele katika sekta ya elimu hasa katika Ujenzi wa miundombinu na kutoa mafunzo Kwa Walimu kazini.

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS