Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Sabasita

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Sabasita, iliyopo Wilayani Bunda Mkoani Mara wakati wa ziara leo Februari 26, 2024.



Wanafunzi hao wameishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kutoa fedha za ujenzi wa Shule hiyo ambayo imeondoa changamoto ya kusafiri umbali mrefu kufuata Elim

Swahili

Prof. James Mdoe amewasili katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya ziara ya Waziri wa Elimu

Naibu katibu Mkuu, Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia anaeshughulikia na elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe amewasili katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya ziara ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof Adolf Mkenda kukagua miradi ya maendeleo katika Chuo hicho.

Swahili

Mradi wa HEET washika kasi - Makubaliano Ujenzi UDSM Lindi, Kagera, Zanzibar Yasainiwa

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omari Kipanga leo Februari 22, 2024 ameshiriki hafla ya utiaji saini ya ujenzi wa majengo 21 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yatakayojengwa mkoani Dar es Salaam, Lindi na Zanzibar pamoja na utiaji saini mkataba wa usimamizi wa ujenzi wa majengo mengine manne yatakayojengwa mkoani Kagera.

Swahili

Tanzania Kubadilishana Uzoefu na Brazil matumizi ya TEHEMA katika Ufundishaji

Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo 2023 inahimiza matumizi ya TEHAMA, Teknolojia na Mifumo mbalimbali ya kibunifu katika Ufundishaji na Ujifunzaji kwa ngazi mbalimbali za Elimu.



Ili Kufikia azma hiyo Tanzania inashirikiana na nchi mbalimbali na kubadilishana uzoefu katika eneo hilo ikiwemo nchi ya Brazil.

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS