Walimu ndio Kitovu cha Mafanikio ya Mitaala Iliyoboreshwa
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amesema kuwa, ili kuwe na mafanikio katika utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mitaala lazima kuwekeza katika kada ya Ualimu.

Prof. Nombo amesema hayo wakati akifungua kikao kazi kati ya Serikali, Shirika lisilo la Kiserikali la Mastercard Foundation na Wadau wa Sekta ya Elimu kwa lengo la kujadili namna ya kuimarisha kada ya ualimu kilichofanyika Machi 18, 2024 Jijini Dar es Salaam.



