VETA, KIST kushirikiana kuimarisha utoaji wa Mafunzo ya Ualimu wa Ufundi na Ufundi Stadi

Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), kupitia Chuo cha Ualimu wa Ufundi Stadi Morogoro (MVTTC), wametia saini hati ya makubaliano ya ushirikiano na Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia (KIST) ya Zanzibar, lengo ni kuimarisha utoaji wa mafunzo ya ualimu wa ufundi na ufundi stadi ili kuzalishaji nguvu kazi yenye ujuzi mahiri sambamba na mabadiliko ya sera ya elimu na mitaala. Mabadiliko haya yanahusisha uanzishwaji wa mchepuo wa Mafunzo ya Amali kuanzia ngazi ya Sekondari, hivyo kusababisha mahitaji makubwa ya walimu wa mafunzo ya ufundi na ufundi stadi.

Swahili

Serikali Imesema ili kukuza Lugha zetu ni lazima Tuendeleze, Tutunze na kuenzi Fasihi Zetu.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda Februari 20, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na washiriki wa Kongamano la Kwanza la Kimataifa Kuhusu Dhima ya Lugha za Asili katika Kujenga Tamaduni - Mtambuka, Diplomasia ya Kiisimu ya Kiuchumi.

Swahili

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan Atunukiwa Tuzo kwa Kutambua Mchango wake katika Kukuza Amani

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akipokea Tuzo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kutambua mchango wake katika kuleta maridhiano nchini iliyotolewa wakati wa Kongamano la Kwanza la Kimataifa la Kukuza Diplomasia ya Kitamaduni, Lugha na Kiuchumi kwa Mustakabali Endelevu linalofanyika Februari 20, 2024 Jijini Dar es Salaam

Swahili

Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango na Prof. Mkenda wamewasili katika Kongamano la Kwanza kuhusu Dhima ya Lugha za Asili katika kujenga Tamaduni- Mtambuka

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda wameshawasili katika Kongamano la Kwanza kuhusu Dhima ya Lugha za Asili katika kujenga Tamaduni- Mtambuka, Diplomasia ya Kiisimu ya Kiuchumi linalofanyika Februari 20, 2024 Jijini Dar es Salaam.

Swahili

Prof. Mkenda anashiriki katika Kongamano la Kwanza la Kimataifa kuhusu Dhima ya Lugha ya Asili katika kujenga Tamaduni - Mtambuka

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda leo Februari 20, 2024 anashiriki katika Kongamano la Kwanza la Kimataifa kuhusu Dhima ya Lugha ya Asili katika kujenga Tamaduni - Mtambuka, Diplomasia ya Kiidimu ya Uchumi linalofanyika jijini Dar es Salaam

Swahili

Prof Mkenda amewasili wilayani Korogwe kwa kufungua Mafunzo ya Kitaifa ya kuwajengea uwezo Walimu Wakuu wa Shule za Msingi kutoka Wilaya ya Korogwe Mji,

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda leo Februari 19, 2024 amewasili wilayani Korogwe mkoani Tanga kwa kufungua Mafunzo ya Kitaifa ya kuwajengea uwezo Walimu Wakuu wa Shule za Msingi kutoka Wilaya ya Korogwe Mji, Korogwe Vijijini na Lushoto wapatao 347, kuhusu Uongozi, Usimamizi wa Shule na Utawala Bora yanayofanyika katika Chuo cha Ualimu Korogwe.

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS