TAARIFA MUHIMU

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imeongeza muda wa Udahili wa Shahada ya Kwanza katika Vyuo vya Elimu ya Juu Nchini. Dirisha la Udahili awamu hii ya Tatu na ya mwisho litafunguliwa kuanzia tarehe 6*hadi 10 Oktoba, 2025

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imeongeza muda wa Udahili wa Shahada ya Kwanza katika Vyuo vya Elimu ya Juu Nchini. Dirisha la Udahili awamu hii ya Tatu na ya mwisho litafunguliwa kuanzia tarehe 6*hadi 10 Oktoba, 2025
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, ameielekeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuhakikisha inaweka mifumo madhubuti ya kuwawezesha walimu kujiendeleza kitaaluma kupitia mafunzo kazini, ili waweze kuendana na mabadiliko ya teknolojia na mahitaji ya sasa ya dunia.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, amesema kuwa chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Serikali imeimarisha mazingira ya walimu kwa kujenga na kuboresha miundombinu ya shule hali iliyoongeza ufanisi wa ufundishaji na ujifunzaji.
Walimu wa Mkoa wa Geita wametoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuthamini kada hiyo na kuwekeza kwa kiwango kikubwa katika sekta ya elimu.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Hussein Omar, amezitaka Taasisi na Mashirika mbalimbali ya elimu kuimarisha usimamizi na uongozi wa elimu ili kuwezesha kikamilifu utekelezaji wa sera ya elimu na Mafunzo ya 2014 Toleo la 2023.
The Government of Tanzania, through the Ministry of Education, Science and Technology, has emphasized that collaboration among universities is a vital source of knowledge, a driver of innovative solutions, and a cornerstone for safeguarding future generations in pursuit of sustainable development.
Bukombe, Geita Tarehe 03 Oktoba 2025, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, anashiriki Maadhimisho ya Siku ya Mwalimu Duniani katika yanayofanyika katika Wilaya ya Bukombe, Mkoa wa Geita.

Aidha, amepata fursa ya kuona shughuli Mbalimbali zinazohusu ustawi wa Walimu katika baadhi ya mabanda ya maony4sho yaliyopo katika viwanja hivyo.