MATUMIZI YA TEKNOLOJIA NI NYENZO KUIMARISHA ELIMU NJE YA MFUMO RASMI
SIKIA HAMASA YA MICHAEL MWAMWI NI MMOJA WA WANUFAIKA 50 WA SAMIA SCHOLARSHIP DS/AI+
PROF. MUSHI ASISITIZA KUANDAA PROGRAMS ZA KUVUTIA NA ZENYE TIJA CHUO KIKUU CHA SUA KAMPASI YA MIZENGO PINDA KATAVI
Naibu Karibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Daniel Mushi Septemba 19, 2025 amekagua maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)
Kampasi ya Mizengo Pinda Katavi.

Mradi huo unatekelezwa chini ya Mradi wa Elimi ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) Kwa gharama ya Sh. bilioni 17.4
TAASISI YA ELIMU YA WATU WAZIMA YAJIPANGA KUFUNGUA MILANGO YA FURSA KWA WOTE
Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Prof. Phillipo Sanga, amesema kuwa Taasisi hiyo imejipanga kuongoza kwa ubunifu na dira pana katika kupanua wigo wa fursa za Elimu Msingi Nje ya Mfumo Rasmi nchini.
MAADHIMISHO YA SIKU YA KISOMO YACHOCHEA ELIMU NJE YA MFUMO RASMI - PROF. MUSHI
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Daniel Mushi, amesema kuwa Maadhimisho ya Siku ya Kisomo Kimataifa na Juma la Elimu ya Watu Wazima yamechochea utekelezaji wa malengo ya Elimu ya Watu Wazima na Nje ya Mfumo Rasmi.
SERIKALI YA TANZANIA YAJIVUNIA KUTEKELEZA MIRADI YA ELIMU YA WATU WAZIMA KWA MAFANIKIO
Serikali ya Tanzania inajivunia kutekeleza miradi mbalimbali kwa mafanikio ikiwemo, mradi wa elimu ya Sekondari Nje ya Mfumo Rasmi, ambapo katika mwaka wa masomo 2025 wanafunzi wapatao 18,886 wavulana 8,648 Wasichana 10239 wamedahiliwa.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Mrindoko katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kisomo Kimataifa na Juma la Elimu ya Watu Wazima Septemba 19, 2025, akimwakilisha Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA KUFIKISHA ELIMU KWA WADAU KUHUSU UTEKELEZAJI WA MIRADI YA NYUKLIA NCHINI
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia TAEC itahakikisha elimu na taarifa kuhusu utekelezaji wa miradi ya nguvu za nyuklia ikiwemo mradi wa kimkakati wa uzalishaji umeme wa nyuklia zinapatikana na kutolewa kwa wadau wote.

Hayo yameelezwa na katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo septemba 2025 Viena Austria katika kikao maalum kati ya Tanzania na Mkuu wa Sehemu ya Maendeleo ya Miundombinu ya Nyuklia wa IAEA, Bi. Liliya Dulinets.
PROF. MUSHI AKAGUA MAANDALIZI YA MAADHIMISHO YA KISOMO KIMATAIFA MPANDA
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Daniel Mushi Septemba 18, 2025 amekagua maandalizi ya Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kisomo Kimataifa na Juma la Elimu ya Watu Wazima yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Kashaulili Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.

Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
WIZARA YA ELIMU YAJA NA MFUMO MPYA WA TAKWIMU ZA ELIMU
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeandaa mfumo wa Takwimu za Elimu ujulikanao kama Education Sector Management Information System (ESMIS). Mfumo huo umeundwa na Wataalamu wa TEHAMA kutoka Wizara hiyo Kwa kushirikiana na Taasisi nyingine ukilenga kuwezesha ukusanyaji, uchambuzi na usimamizi wa takwimu muhimu za sekta ya elimu.

