DKT. HUSSEIN OMAR KATIKA HAFLA YA KUZINDUA TAARIFA YA TATHMINI YA SERA ZA UREJEAJI SHULENI

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Hussein Mohamed Omar, katika halfa ya Uzinduzi wa Taarifa ya Tathimini ya Sera za Urejeaji na Mpango wa Utekelezaji wa Mwongozo wa kuwarejesha Shuleni Wanafunzi waliokatiza masomo katika Elimu ya Msingi na Sekondari kwa sababu mbalimbali Novemba 12, 2025 jijini Dar es Salaam.

Swahili

TENMET YAPONGEZA USHIRIKIANO BAINA YA SERIKALI NA WADAU WA ELIMU

Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bi. Martha Makala, ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kuongeza wigo wa ushirikiano na wadau mbalimbali wa elimu hatua ambayo imeimarisha mahusiano na kuchochea utekelezaji wa kazi mbalimbali.



Bi. Makala amesema hayo Novemba 12, 2025 jijini Dar es Salaam katika hafla ya Uzinduzi wa Mpango wa utekelezaji Mwongozo wa kuwarejesha Shuleni Wanafunzi waliokatiza masomo katika Elimu ya Msingi na Sekondari.

Swahili

SERIKALI YADHAMIRIA KUBORESHA UPANGAJI WA WATUMISHI SEKTA YA ELIMU KUPITIA MFUMO WA e-MSAWAZO

Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Taasisi kutoka Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mh. Nolasco Jacob Kipanda, ambaye alikuwa mgeni rasmi, amepongeza Wizara ya Elimu kwa kujielekeza kwenye matumizi ya mifumo ya kidijitali ili kuboresha usimamizi wa rasilimali watu.

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS