VIJANA WA TANZANIA WANG’ARA KATIKA UANDISHI WA INSHA ZA EAC NA SADC
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Dkt. Hussein Omari, amesema Serikali itaendelea kuwekeza katika kukuza vipaji vya vijana kupitia elimu, akisema juhudi hizo zinawajenga kuwa kizazi kinachofikiri kwa kina na chenye mchango kwa taifa.


