DKT. HUSSEIN OMAR AFUNGA KIKAO CHA PAMOJA CHA SERIKALI NA BENKI YA DUNIA KUHUSU MIRADI YA SEQUIP NA BOOST

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Hussein Mohamed Omar amefunga Kikao cha Pamoja kati ya Serikali na Benki ya Dunia (Joint Mission Meeting) kuhusu utekelezaji wa Miradi ya Kuimarisha Ubora wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) na Mpango wa Kuboresha Elimu ya Awali na Msingi (BOOST).

Swahili

UJUZI WA VIJANA NGUZO YA UCHUMI WA VIWANDA

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera, amesema kuwa sekta ya viwanda ndiyo injini ya uchumi wa taifa, lakini injini hiyo haiwezi kukimbia bila mafuta ya ujuzi.

Akizungumza Oktoba 17, 2025 jijini Dar es Salaam katika mkutano wa VETA, wamiliki wa viwanda, waajiri na wadau wa elimu ya ufundi stadi, Dkt. Serera amesisitiza kuwa ushirikiano kati ya VETA na sekta ya viwanda si wa hiari, bali ni wajibu wa kitaifa katika kuinua uchumi wa taifa.

Swahili

SERIKALI YAENDELEA KUWEKEZA KATIKA MAFUNZO YA UFUNDI NA UFUNDI STADI

Serikali inaendelea kuwekeza katika elimu ya ufundi na ufundi stadi ili kuandaa vijana wenye ujuzi, umahiri na ubunifu unaokidhi mahitaji ya soko la ajira. Akizungumza Oktoba 17, 2025 jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, amesema mfumo wa elimu unalenga kuandaa wahitimu wenye ushindani wa kimataifa na uwezo wa kujiajiri au kuajiriwa ndani na nje ya nchi.

Swahili

TANZANIA YAIMARISHA MATUMIZI YA TEHAMA KATIKA UJIFUNZAJI

Serikali inaendelea kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika ujifunzaji na ufundishaji katika ngazi zote za elimu nchini kuanzia elimu ya awali hadi vyuo vikuu.



Hayo yameelezwa leo tarehe 16 Oktoba 2025 na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Hussein Mohamed Omar alipokutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Imagine World Tanzania Dkt. Jacqueline Mgumia katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma

Swahili

PROF. MUSHI ASHIRIKI MKUTANO WA KITAIFA WA MARKUP II KWA UKUAJI WA MASOKO YA MAZAO YA KIMKAKATI

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Daniel Mushi, Oktoba 15, 2025 jijini Dodoma ameshiriki Mkutano wa Tatu wa kitaifa wa Kamati ya Makatibu Wakuu kuhusu Mradi wa Uongezaji Thamani na kukuza Masoko ya Ndani na Nje ya Nchi (MARKUP II) ya mazao ya kimkakati.

Swahili

KAMPASI YA NJOMBE KUCHOCHEA MAENDELEA YA ELIMU NA UCHUMI NYANDA ZA JUU KUSINI

Na WyEST, Njombe

Kuanzishwa kwa Kampasi ya Njombe ya Chuo Kikuu cha Dodoma kupitia Mradi wa HEET kumeanza kutaleta mabadiliko makubwa katika sekta ya elimu, ajira na uchumi wa mkoa wa Njombe. Mradi huu unalenga kuongeza fursa za elimu ya juu kwa vijana wa Kusini na kuchochea maendeleo ya miundombinu ya kisasa.

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS