DKT. MWIGULU AKUTANA NA PROF. MKENDA NA TIMU YA WATAALAM YA WIZARA YA ELIMU

Waziri Mkuu, Dkt.Mwigulu Nchemba leo Januari 15, 2026 amefanya kikao cha kazi na Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda (wa pili kulia), Naibu Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia, Wanu Hafidh Ameir, pamoja na Timu ya Wataalam kutoka Wizara hiyo.



Kikao hicho ambacho kimefanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma pamoja na mambo mengine wamejadili mikakati mbalimbali yenye lengo la kuendeleza sekta ya elimu nchini.

Swahili

MKAKATI WA KITAIFA WA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KUCHOCHEA UJIFUNZAJI KIDIJITALI

Mkakati wa Kitaifa wa Matumizi ya Teknolojia za Kidijitali katika elimu umezingatia ubora wa elimu, usawa wa fursa, ubunifu, na matumizi yanayolengwa ya teknolojia za kidijitali Nchini.



Kauli hiyo imetolewa Januari 14, 2026 jijini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Daniel Mushi akizungumza katika Warsha ya kujenga uelewa wa pamoja juu ya Mkakati wa Kitaifa wa Matumizi ya Teknolojia za Kidijitali katika Elimu na Miongozo yake.

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS