SERIKALI YAZINDUA MKAKATI WA KISAYANSI WA KUSOMA, KUANDIKA NA KUHESABU KWA WATOTO WA TANZANIA

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejipanga kuimarisha umahiri wa kusoma, kuandika na kuhesabu kwa watoto wa elimu ya awali na wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili. Kupitia Mkakati wa Kisayansi, hatua hii inalenga kuweka msingi thabiti wa maarifa na ujuzi wa msingi, ili kuhakikisha kila mtoto anapata nafasi ya kujengewa uwezo wa kitaaluma na kiujuzi mapema.

Swahili

WAZIRI MKENDA AWAALIKA WATANZANIA KWENYE UZINDUZI WA MKAKATI WA KISAYANSI WA ELIMU MSINGI

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Carolyne Nombo, tarehe 28 Januari 2026 kupitia Televisheni ya Taifa (TBC1), wamewaalika Watanzania kushiriki katika uzinduzi wa Mkakati wa Kisayansi wa Kujenga Umahiri wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu kwa watoto wa Elimu ya Awali na wanafunzi wa Darasa la Kwanza na la Pili.

Swahili

SERIKALI YABORESHA MFUMO WA MIKOPO YA ELIMU YA JUU KUPITIA TEKNOLOJIA YA AKILI BANDIA

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Daniel Mushi, amesema Serikali kupitia wizara hiyo inaendelea kusimamia kwa karibu mapitio ya muundo na mfumo wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), kwa lengo la kuboresha mifumo ya upangaji na utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.

Swahili

PROF. NOMBO AKUTANA NA MKURUGENZI WA FCDO KUJADILI USHIRIKIANO WA ELIMU

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, tarehe 27 Januari 2026, amekutana na Ms Anna Wilson, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Rasilimali Watu kutoka Ofisi ya Mambo ya Nje, Jumuiya ya Madola na Maendeleo ya Uingereza (FCDO).



Lengo la kikao hicho kilikuwa ni kujitambulisha pamoja na kumpitisha mgeni huyo katika majukumu na kazi mbalimbali zinazotekelezwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia katika kuendeleza sekta ya elimu nchini.

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS