PROF. MKENDA AKAGUA MAANDALIZI YA UZINDUZI WA JENGO LA TAALUMA ZANZIBAR

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda Januari 8, 2026 Visiwani Zanzibar akikagua maandalizi ya uzinduzi wa Jengo la Taaluma na Utawala la Taasisi ya Sayansi za Bahari
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM-IMS) eneo la Buyu Wilaya ya Mjini Magharibi B, Zanzibar litakalozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu

Swahili

FURSA KWA VIJANA, MHE SHAYO KUFADHILI MASOMO YA VIJANA 10 KILA MWAKA VETA MOSHI

Katika kuunga mkono juhudi za Serikali, zinazotekelezwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na wadau katika kuimarisha Elimu Amali, Mbunge wa Moshi Mjini, Mhe. Ibrahim Shayo, ameahidi kufadhili masomo ya vijana 10 kila mwaka katika Chuo cha VETA Moshi.



Mhe. Shayo ametoa ahadi hiyo Januari 07, 2026 mkoani Kilimanjaro baada ya kujionea mafanikio ya chuo hicho katika kutoa elimu ya vitendo inayowawezesha vijana kupata ajira ndani na nje ya nchi.

Swahili

MHE. WANU AITAKA VETA MOSHI KUIMARISHA USHIRIKIANO NA MAKAMPUNI KWA AJILI YA AJIRA NA TEKNOLOJIA MPYA

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir, ameielekeza VETA Moshi kuimarisha ushirikiano na makampuni na viwanda ili kuongeza ajira kwa wahitimu na matumizi ya teknolojia mpya, kwa kuzingatia uelekeo wa nchi kama ulivyoainishwa katika Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050, sera za kisekta na miongozo mbalimbali ya kitaifa.

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS