SERIKALI YAENDELEA KUGHARIMIA ELIMU YA UFUNDI, DIT SONGWE YATAJWA KUWA KICHOCHEO CHA MAENDELEO
SKAUTI INADUMISHA MSHIKAMANO NA USTAWI WA VIJANA KITAIFA - WAZIRI MKENDA
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, ambaye pia ni rais wa Chama cha Skauti Tanzania Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa chama hicho kinasaidia kujenga mshikamano wa vijana, kukuza maadili na uzalendo kwa vijana Nchini.

Waziri Mkenda ameeleza hayo Januari 9, 2026 Mkoani Pwani akifungua Mkutano wa 7 wa chama hicho, akisisitiza kuwa, Wizara itaendelea kuimarisha uskauti katika taasisi za elimu ili kiendelee kujenga ustawi wa nchi.
TANZANIA, UAE KUJADILI USHIRIKIANO WA KIMKAKATI KATIKA ELIMU NA SAYANSI
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu, ameongoza majadiliano kati ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Balozi wa Falme za Kiarabu (UAE) nchini, Mhe. Khalifa Abdulrahman Almarzouqi, kuhusu kuimarisha ushirikiano wa kielimu kati ya nchi hizo mbili.
PROGRAM ZA ELIMU YA JUU NA KATI ZIZINGATIE MALENGO YA MSINGI YA CHUO - MHE. AMEIR
FURSA KWA VIJANA, MHE SHAYO KUFADHILI MASOMO YA VIJANA 10 KILA MWAKA VETA MOSHI
NAIBU WAZIRI WANU AMEIR AELEKEZA VETA MOSHI KUIMARISHA USHIRIKIANO NA VIWANDA KWA AJIRA
SERIKALI YAENDELEA KUGHARIMIA ELIMU YA UFUNDI, DIT SONGWE YATAJWA KUWA KICHOCHEO CHA MAENDELEO
Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika elimu ya ufundi nchini ikiwemo kugharimia chakula na mafunzo kwa vitendo viwandani kwa maelfu ya wanafunzi, ili kuzalisha rasilimaliwatu yenye ujuzi unaokidhi mahitaji ya soko la ajira na kuchochea maendeleo ya Taifa.
MAGEUZI YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA KUJENGA UCHUMI IMARA NA ENDELEVU - MHE. SAMIA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali imedhamiria kufanya mageuzi ya elimu, sayansi, utafiti na ubunifu ili kujenga uchumi imara na endelevu.

Mhe. Samia amesema hayo Januari 8, 2026 baada ya kuzindua Jengo la Taaluma na Utawala la Taasisi ya Sayansi za Bahari Zanzibar Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM - MSI). Amesisitiza kuwa Taasisi hiyo, ni mdau muhimu kwa Serikali katika kujenga uchumi shindani na shirikishi.
RAIS SAMIA AKAGUA JENGO LA TAALUMA NA UTAWALA UDSM-IMS ZANZIBAR
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Januari 8, 2026 amekagua Jengo la Taaluma na Utawala la Taasisi ya Sayansi za Bahari Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM-IMS) lililopo eneo la Buyu Wilaya ya Mjini Magharibi B, Visiwani Zanzibar.


