Taarifa kwa Umma
MKENDA AVALIA NJUGA SUALA LA SHULE YA WANAFUNZI 1,500 KUKOSA VYOO
SERIKALI KUENDELEA KUTOA KIPAUMBELE KWA WANAOSOMA MASOMO YA SAYANSI
Bwana Ametoa, Bwana ametwaa Jina lake Lihimidiwe
Prof. Nombo amekutana na Watumishi wa WyEST katika Kikao Kazi cha mwaka kujadili masuala mbalimbali ya Wizara hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo leo Februari 14, 2024 jijini Dodoma amekutana na Watumishi wa Wizara hiyo katika Kikao Kazi cha mwaka kujadili masuala mbalimbali ya Wizara hiyo.

Awali katika salamu za Ufunguzi wa kikao kazi hicho Prof. Nombo ameeleza kuwa mafanikio yanayoonekana katika Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yametokana na juhudi za Watumishi wote ambao wamewajibika kikamilifu.
Bilioni 6.53 kujenga Chuo cha VETA cha Mkoa wa Songwe kitakachokuwa na majengo 25
Mhe. kipanga yupo Abu Dhabi kushiriki Mkutano wa UNESCO kuhusu Elimu ya Utamaduni na Sanaa
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omari Kipanga yupo Abu Dhabi, Falme za Kiarabu kwa lengo la kushiriki Mkutano wa UNESCO kuhusu Elimu ya Utamaduni na Sanaa.

Mkutano huo wa siku tatu ulioanza tarehe 13 hadi 15 Februari 2024, utatoa fursa kwa wajumbe kutoka nchi wanachama kupitishwa katika Kiunzi cha Elimu ya Utamaduni na Sanaa ( Framework for Culture and Arts Education).
Serikali kuendelea kutoa Kipaumbele kwa Wanaosoma Masomo ya Sayansi
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema Serikali inaendelea kutoa kipaumbele kwa wanaosoma masomo ya Sayansi ikiwemo kutoa ufadhili wa masomo ili kuongeza hamasa kwa Vijana wa kitanzania wakiwemo wasichana kupenda kusoma masomo hayo.


