Prof. Carolyne Nombo amekabidhi magari kwa NECTA, TET na ADEM
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo leo Januari 26,2024 amekabidhi magari kwa Baraza la Mitihani Tanzania, Taasisi ya Elimu Tanzania na Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu kwa ajili ya kuhakikisha ufatiliaji wa utekelezaji wa shughuli za elimu nchini

Prof. Nombo amekagua Studio mpya iliopo katika Ofisi za Taasisi ya Elimu Tanzania
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo leo Januari 26, 2024 amekagua Studio mpya iliopo katika Ofisi za Taasisi ya Elimu Tanzania ambazo zitatumika kuandaa vipindi vya elimu kwa umma kuhusu masuala mbalimbali ya sekta ya elimu

MATOKEO YA MTIHANI WA TAIFA WA KIDATO CHA NNE NA MAARIFA ULIOFANYIKA NOVEMBA 2023.
Ndejembi ashuhudia Majaribio ya Mfumo wa Smart Classroom kukabiliana na Uhaba wa Walimu
Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Deogratius Ndejembi ametembelea na kuzindua majaribio ya mfumo wa ufundishaji mubashara "Live Teaching" ambao utawezesha wanafunzi wa shule mbalimbali nchini kuunganishwa na mwalimu anayefundisha katika shule ya Sekondari Kibaha ili kukabiliana na changamoto ya uhaba walimu nchini.
Prof Mkenda anena siku ya Elimu Duniani
Prof. Mkenda ameungana na viongozi mbalimbali kushiriki kikao kati ya Makamu wa Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango na Makamu wa Rais wa Cuba
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda leo Januari 24,2024 ameungana na viongozi mbalimbali kushiriki kikao kati ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango na Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Salvador Mesa, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mhe. Kipanga amekutana Mkurugenzi wa Shirika la Nutrition International Dr. George Mwita
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia amekutana na Uongozi wa Shirika la Nutrition International ukiongozwa na Mkurugenzi wa Shirika hilo Dr. George Mwita.

Viongozi hao wamefika kutambulisha Shirika hilo na miradi wanayotekeleza inayogusa sekta ya Elimu ambapo walengwa wake wakuu ni vijana wa umri wa balehe ambao wengi wao ni wanafunzi.
Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara Bw. Atupele Mwambene.

