SERIKALI YASISTIZA UTEKELEZAJI WA SERA YA ELIMU NA UREJEAJI WA WANAFUNZI SHULENI
Waratibu elimu kata na wakuu wa shule za msingi na sekondari wametakiwa kusimamia kikamilifu utekelezaji wa mwongozo wa urejeaji wa wanafunzi waliokatisha masomo pamoja na Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 (Toleo la 2023), ili kuhakikisha hakuna mtoto anayebaki nje ya mfumo wa elimu.

