Mtanzania Ashika Nafasi ya pili Tuzo za Ubunifu Afrika

Mtanzania Mariam Mhina kutoka kampuni ya TAI Impact Tanzania ameshinda nafasi ya pili kwenye tuzo za ubunifu kwenye Elimu katika Africa Skills Week iliyofanyika Accra Ghana 14 - 18 Oktoba 2024.

Mariam Mhina aliingia katika mashindano yaliyohusisha wabunifu 611 kutoka nchi mbalimbali za Afrika na kufuzu kufikia kwenye wabunifu 10 bora na kwenda kushinda nafasi ya pili.

Swahili

Kamati ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDC) imekutana kupokea, Kujadili na kupitisha miongozo mbalimbali ya Elimu

Kamati ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDC) leo Oktoba 18, 2024 imekutana Jijini Dodoma kupokea, Kujadili na kupitisha miongozo mbalimbali ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.



Kikao hicho kimeongozwa na Naibu Katibu Mkuu anaeshughulikia Sayansi Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Daniel Mushi akiwa na Wenyeviti wenza Naibu Katibu Mkuu Elimu Ofisi ya Rais- Tamisemi Atupele Mwambene, Mwakilishi wa UNICEF Simone Vis na Mwenyekiti wa TENMET Faraja Nyalandu.

Swahili

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni, na Michezo imeendelea na vikao kupokea taarifa

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni, na Michezo imeendelea na vikao kupokea taarifa mbalimbali.



Leo Oktoba 17, 2024 jijini Dodoma Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imewasilisha taarifa ya Utendaji Kazi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) na Taarifa ya maendeleo ya Ujenzi wa Vyuo vya Ufundi Stadi na Chuo cha VETA Mkoa wa Songwe.

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS