MRADI WA HEET KUIWEZESHA TAASISI YA SAYANSI ZA BAHARI KUONGEZA UDAHILI NA PROGRAMU ZA MAFUNZO
Timu ya Benki ya Dunia Oktoba 28, 2024 imeendelea na ziara yake ya kukagua Miradi inayotekelezwa na Taasisi za Elimu ya Juu kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Maendeleo ya Kiuchumi (HEET) unaofadhiliwa na benki hiyo.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa Mradi huo katika Kampasi ya Buyu, Mratibu Msaidizi Dkt. Libereta Haule amesema kuwa mradi umewezesha kuongeza udahili wa wanafunzi katika kampasi hiyo ya awali kutoka 139 hadi kufikia 278.


