SERIKALI IPO TAYARI KUSHIRIKIANA NA WADAU KUBORESHA MITAALA YA MAFUNZO YA UANDISHI WA HABARI

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa Serikali ipo tayari kukaa na wadau wa Habari ili kupata maoni juu ya uboreshaji mitaala ya mafunzo ya uandishi wa habari.



Akizungumza Novemba 01, 2024 Mkoani Singida katika Mkutano wa Mwaka wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) amesema kuwa lengo la kufanya mapitio hayo ni kuwezesha mafunzo ya uandishi wa habari yaweze kuendana na mabadiliko ya teknolojia.

Swahili

PROF. MKENDA AKUTANA NA NZIMANDE WAZIRI WA ELIMU AFRIKA KUSINI

#Tanzania na Afrika kusini kushirikiana kuimarisha Sayansi, Teknolojia na Ubunifu



Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amekutana na Waziri wa Elimu ya Juu Sayansi, Teknolojia na Ubunifu wa Afrika Kusini Mhe. Dkt. Blade Nzimande ambapo wamejadili namna ya kuimarisha uhusiano katika nyanja za Sayansi, Teknolojia na Ubunifu.

Swahili

SHULE ZA SEKONDARI ZA SIMIYU NA DODOMA KUFAIDIKA NA UFADHILI KUTOKA KOICA

Shule za Sekondari za Simiyu na Dodoma kufaidika na ufadhili wa dola za kimarekani milioni 10 kutoka Shirika la Maendeleo la Korea Kusini (KOICA) kwenye ujenzi wa maabara za kisasa za sayansi na TEHAMA. Mradi huo unatarajiwa kutekelezwa kwa miaka 3.

Hayo yamejiri wakati wa ziara ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo, na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Ndugu Atupele Mwambene nchini Korea Kusini kwa ajili ya maandalizi ya mradi huo.

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS