VIJANA 12,000 WALIOKUWA NJE YA MFUMO RASMI WA WLIMU WAREJESHWA
ELIMU YA WATU WAZIMA INACHOCHEA MAENDELEO YA WATANZANIA
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amesema Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi ina mchango mkubwa katika kuwezesha wananchi kupata maarifa, ujuzi na mielekeo stahiki kwa maendeleo endelevu.

Prof. Nombo ametoa kauli hiyo Oktoba 10, 2024 Mkoani Tabora akifungua Kongamano la Wadau wa elimu ambapo amesema Serikali inatambua kinadharia na vitendo umuhimu wa Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi.
Prof. Mushi ahimiza kasi utekelezaji Mradi wa HEET
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Daniel Mushi amewataka waratibu wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET),kuongeza kasi ya mchakato wa manunuzi pamoja na kusimamia fedha kwa weledi,ili zifanye kazi iliyo kusudiwa.

