Serikali inaendelea kutekeleza Program za Elimu ya Watu Wazima kuhakikisha inatoa fursa ya Elimu kwa wote.

Afisa Elimu Mkoa wa Tabora Mwl. Upendo Rweyemamu amesema Serikali Mkoani humo inaendelea kutekeleza program za elimu ya Watu Wazima kuhakikisha inatoa fursa ya elimu kwa wote.



Akizungumza katika Kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Juma la Elimu ya Watu Wazima Upendo amesema Mkoa huo umefanikiwa kutekeleza program ya Mpango wa Elimu Changamani kwa Vijana walio nje ya Shule (IPOSA) ambayo mpaka sasa ina vituo 40 vyenye Wanafunzi 1,041.

Swahili

Elimu ya Watu Wazima inasaidia kukuza maarifa ya mtu mmoja mmoja

Mratibu masuala ya elimu kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) Dkt. Ayoub Kafyulilo amesema elimu ya Watu Wazima inasaidia kukuza maarifa ya mtu mmoja mmoja kuwawezesha kushiriki katika sekta mbalimbali za uzalishaji.



Dkt. Kafyulilo amesema hayo Oktoba 11, 2024 Mkoani Tabora ambapo amesema kuwa jamii iliyoelimika, inasaidia kuwa na kizazi chenye maarifa na ujuzi.

Swahili

Prof. Adolf Mkenda akutana na wanafunzi wa Sekondari wanaojivunia Elimu Amali

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda Oktoba 11, 2024 akutana na wanafunzi wa Sekondari wanaojivunia Elimu Amali katika Shule ya Sekondari ya Iluhya Mkoani Kagera



Wanafunzi hao walimtembeza Waziri Prof. Mkenda katika Shamba, bustani na eneo wanalofugia mbuzi na kumpatia maelezo ya namna wanavyoendesha shughuli hizo

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS