WATAALAM WA LUGHA KUTOKA CUBA WAANZA KUFUNDISHA KIHISPANIA SUA, WAONGEZA NGUVU KATIKA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimepokea wataalam wawili wa lugha kutoka nchini Cuba, watakaofundisha lugha ya Kihispania kwa kipindi cha miaka miwili chini ya Idara ya Lugha, katika jitihada za kuendeleza elimu ya kimataifa na kuboresha umahiri wa lugha miongoni mwa wanafunzi.

Swahili

ESWATINI WAJA TANZANIA ZIARA YA MAFUNZO YA ULINGANIFU KATIKA SEKTA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imepokea ujumbe wa wataalamu kutoka Falme ya Eswatini ambao wapo katika ziara ya mafunzo ya ulinganifu, inayoratibiwa na taasisi ya Economic Policy and Analysis Research Centre (ESEPARC) kwa kushirikiana na Wizara ya Kazi na Hifadhi ya Jamii (MoLSS) ya Falme ya Eswatini.

Swahili

MAJALIWA ATOA WITO WA USHIRIKIANO KUJENGA TAIFA LENYE WATU WENYE UJUZI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa, amesema Serikali itaendelea kuimarisha nguvu kazi yenye ujuzi ili iweze kushindana katika soko la ajira la ndani na kimataifa.



Mhe. Majaliwa amesema hayo 11 Oktoba 2025 jijini Dar es Salaam, wakati akifungua Kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS