Prof. Nombo akabidhiwa Uenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya AICAD - Jijini Dodoma
Swahili
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo leo Oktoba 5, 2023 amekabidhiwa Uenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Afrika (AICAD) inayohusika kujengea uwezo Vyuo Vikuu na Jamii katika masuala mbalimbali ikiwemo Kilimo, maji na kuongeza thamani.
Prof. Nombo anapokea nafasi hiyo kutoka Kenya kwa ajili ya kuongoza kwa miaka miwili kuanzia mwaka 2023.
