Elimu ya Watu Wazima ni Nguzo ya Msingi kwa jamii Kuleta Maendeleo Endelevu

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema Serikali kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali nchini wameendelea kutumia Elimu ya Watu Wazima katika nyanja mbalimbali ili kuisadia jamii kukabiliana na changamoto zilizopo.

Prof. Mkenda ametoa kauli hiyo Oktoba 13, 2023 wakati akihitimisha Kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Juma la Elimu ya Watu Wazima lililofanyika Maili Moja, Kibaha Mkoani Pwani, ambapo ametumia fursa hiyo kupongeza jitihada hizo zinazoendelea kuwakomboa wananchi kuweza kupata elimu na  ujuzi.

Swahili

Dkt. Naomi Katunzi Aishukuru Serikali kupitia Mradi WA SEQUIP, kwa kuipatia Taasisi hivyo Fedha kwa ajili ya Ujenzi na Ukarabati wa Madarasa na Vituo vya Elimu.

Mwenyekiti wa Baraza la Usimamizi wa Taasisi ya Elimu Watu Wazima (TEWW) Dkt. Naomi Katunzi ameishukuru serikali kupitia Wizara ya Elimu chini ya Mradi WA SEQUIP, kwa kuipatia taasisi hivyo jumla ya fedha TZS. Bilioni 5.7 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa madarasa na vituo vya Elimu.

Dkt. Katunzi ametoa pongezi hizo Oktoba 12, 2023 wakati akizungumza kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Juma la Elimu ya Watu wazima Viwanja vya Maili Moja Wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani.

Swahili

Serikali Inaendelea Kuimarisha Utolewaji wa Elimu ya watu Wazima na Elimu nje ya Mfumo Rasmi

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Elimu Msingi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Ndg. Josephat Luoga amesema Serikali kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo imekuwa ikitekeleza program na Mipango mbalimbali ya Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi kwa lengo la kuwa na Watanzania walioelimika na wenye uwezo wa kushiriki katika shughuli za maendeleo yao binafsi na Taifa kwa ujumla.

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS