Prof. Nombo Akutana na Kansela Mkuu wa Ushirikiano na Maendeleo kutoka ubalozi wa Canada hapa nchini
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Nombo leo Oktoba 12, 2023 jijini Dar es Salaam amekutana na kufanya mazungumzo na Bi. Helen Fytche, Kansela Mkuu wa Ushirikiano na Maendeleo kutoka ubalozi wa Canada hapa nchini ambae ameambatana na Bi. Rasmata Barry, muambata wa masuala ya maendeleo ya elimu.
Mazungumzo yamelenga kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Canada na kuona namna ya kuanzisha maeneo mapya ya ushirikiano katika Sekta ya elimu.


