Prof. Mkenda Awasili Viwanja vya Satellite City, Killipo Chuo cha Ufundi Stadi Veta Wilaya ya Igunga

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda tayari awasili Viwanja vya Satellite City Nkokoto A, Killipo Chuo cha Ufundi Stadi Veta Wilaya ya Igunga mkoani Tabora kwa ajili ya kukagua hatua mbalimbali za maandalizi ya uwekaji jiwe la Msingi la Ujenzi wa Chuo hicho.

Swahili

Prof. Nombo atembelea Viwanja vya Satellite City kukagua maandalizi ya uwekaji jiwe la Msingi la Ujenzi wa Chuo cha VETA Wilaya ya Igunga

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo mapema leo atembelea Viwanja vya Satellite City Nkokoto A, kukagua maandalizi ya uwekaji jiwe la msingi la Ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi Veta Wilaya ya Igunga mkoani Tabora.

Swahili

Mkuu wa Mkoa Tanga Afungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Elimu

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Waziri Kindamba ameipongeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kazi kubwa inayofanya katika kuhakikisha nchi inakuwa na Sera na Mitaala itakayowezesha watanzania kupata elimu bora.

Ametoa pongezi hizo Oktoba 16, 2023 Mkoani Tanga wakati akifungua Mkutano wa 32 wa Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo ambapo amewataka watumishi hao kuendelea kushirikiana na kufanya kazi kwa bidii, weledi na nidhamu ilikuleta ufanisi katika kuhakikisha elimu inayotolewa inakuwa katika viwango vya ushindani kitaifa, kikanda na kimataifa

Swahili

Rais Samia Azindua Shule za Mradi wa BOOST wa Tril. 1.5/-

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua shule za Msingi zilizojengwa na Mradi wa kuimarisha Shule za Awali na Msingi (BOOST) katika shule ya Msingi Imbele iliyojengwa katika Manispaa ya Singida mkoani Singida kwa niaba ya shule zote zinazojengwa mradi wa huo.

Dkt. Samia amezindua shule hiyo tarehe 15.10.2023 wakati wa ziara yake mkoani Singida.

Amesema amezindua mradi huu ni kwa niaba ya miradi mingine yote kama hii inayojengwa nchini kote ambayo inasaidia watoto waweze kupata elimu bora.

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS