Wizara ya Elimu yakutana na Wamiliki wa Shule
Wamiliki wa Shule zisizo za Serikali wakichangia mada
Wamiliki wa Shule zisizo za Serikali wakichangia mada mbalimbali juu ya namna bora ya kuwezesha uwekezaji katika elimu ili kuwezesha watoto wa kitanzania kupata elimu bila changamoto yeyote

Wizara na Wamiliki wa Shule Zisizo za Serikali Wakutana Kujadili Changamoto katika Elimu
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imefanya mkutano na Wamiliki wa Shule zisizo za Serikali kwa lengo la kusikiliza na kujadiliana kwa pamoja changamoto zilizopo katika sekta hiyo.
Akizungumza Oktoba 10, 2023 jijini Dodoma, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema mkutano huo ni wa Kihistoria kwani kwa mara ya kwanza unafanyika ikiwa ni ushirikishwaji wa Sekta Binafsi na unalenga kusikiliza changamoto katika uwekezaji, uendeshaji wa shule na kuona namna ya kusaidia kuzitatua na kuweka mikakati ya pamoja.
Mkutano wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Wamiliki wa shule zisizo za Serikali
Serikali Kupitia Mradi wa SEQIUP kuwezesha Ujenzi wa shule 15 mpya za Sekondari - Mkoa wa Mbeya
Hongera Mhe. Samia Suhluhu Hassan
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru kwenye hafla iliyofanyika New Delhi nchini India tarehe 10 Oktoba, 2023.
Rais Samia ni Mwanamke wa Kwanza kutunukiwa Shahada hiyo ya Heshima na Chuo hicho nchini India. Ni Viongozi wawili tu ambao wametunukiwa Shahada hiyo ya Heshima akiwemo Rais wa Urusi Mhe. Vladmir Putin pamoja na Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Japan Hayati Shinzo Abe.
Vyuo Vikuu Vyatakiwa Kufanya Tafiti zenye Tija Kuchochea Ushindani katika Ugunduzi
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema Vyuo vikuu havipimwi kwa wingi wa wanafunzi na mapato badala yake tafiti inazofanya zenye kuleta gunduzi, kukuza maarifa na ujuzi katika jamii
Prof. Mkenda amesema hayo jijini Dodoma wakati akizindua Baraza jipya la Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na kutoa wito kwa Vyuo vikuu kuzingatia ufanyaji wa tafiti zenye tija nchini ili kuchochea ushindani katika gunduzi mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Tunaipongeza Tanzania kuchukua kofia ya Uenyekiti wa bodi AICAD Prof. Byarugaba
Tanzania Uholanzi kuimarisha ushirikiano sekta ya Elimu.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo Oktoba 6, 2023 jijini Dodoma amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Rotterdam nchini Uholanzi ukiongozwa na Prof Peter Knorringa kutoka uholanzi.

