Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo Yaridhishwa na Utekelezaji wa Mradi wa EASTR ATC

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, Mhe. Husna Juma Sekiboko, amekipongeza Chuo cha Ufundi Arusha kwa usimamizi mzuri wa utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa Kituo cha Umahiri cha Nishati Jadidifu katika kampasi ya kikuletwa.

Kampasi hiyo iliyopo Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro, kupitia ufadhili wa mradi wa Ujuzi na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (EASTRIP) inajenga miundombinu mbalimbali ya kufundishia na kujifunzia.

Swahili

Rais Samia Akutana na Wanafunzi wa St. Mary's Tabora

# Shule ya kwanza ambayo Mwl. Nyerere alifundisha

# Wanafunzi waguswa ujio wake

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Oktoba 18, 2023
azungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari St. Mary's iliyopo mkoani Tabora, wakati alipokwenda kumtembelea Askofu Mkuu Mwandamizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Tabora Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa.

Swahili

Serikali Yadhamiria kukuza Ujuzi kwa Vijana kupitia Mafunzo ya Amali - Rais Samia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inaendelea na dhamira ya kukuza ujuzi kwa vijana wa kitanzania Kwa sababu wao ndio nguvu kazi ya Taifa.

Rais Samia ametoa kauli hiyo hii leo Oktoba 17, 2023 katika Viwanja vya Barafu wilayani Igunga baada ya kuweka jiwe la msingi Ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi kilichopo wilayani humo mkoani Tabora.

Swahili

Prof. Mkenda Ateta na Vijana wa Hamasa Mkoani Tabora

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ateta na Vijana wa hamasa mkoani Tabora awahimiza kutumia fursa vizuri ya Mafunzo katika Chuo cha Ufundi Stadi kilichopo wilayani Igunga pindi kitakapoanza kutoa mafunzo ya amali katika kozi mbalimbali ikiwemo kilimo na ufugaji.

Prof. Mkenda ametoa ushauri huo hii leo Oktoba 17, 2023 wakati akizungumza na makundi mbalimbali juu ya mageuzi tarajiwa katika Elimu , mazungumzo hayo yalisheheni faida lukuki kwa vijana na Taifa kwa ujumla.

Swahili

Prof. Nombo Asema Serikali Inatekeleza Mipango na Miradi ya Elimu kupitia Vyuo vya Ufundi Stadi

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amesema Serikali inaendelea kutekeleza kwa ufanisi mkubwa mipango na Miradi ya Elimu kupitia Vyuo vya Ufundi Stadi ili kuhakikisha Taifa linapata Vijana mahiri na wenye Ujuzi watakaoweza kulikabili soko la Ajira ndani na nje ya nchi.

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS