Prof. Mkenda atazindua ufadhili kwa Wanafunzi wa Kike wanaosoma programu za Uhandisi katika sekta ya usafirishaji na kuweka jiwe la msingi

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda leo Oktoba 28, 2023 atazindua ufadhili (Scholarship) kwa Wanafunzi wa Kike wanaosoma programu za Uhandisi katika sekta ya usafirishaji pamoja na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa majengo matano ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji yanayofadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia Mradi wa Kujenga Ujuzi na Ushirikiano wa Kikanda wa Afrika Mashariki (EASTRIP).

Swahili

Tanzania na Canada kutekeleza Mradi wa Bilioni 45 wa uwezeshaji na mafunzo ya Ujuzi

Na WyEST
Dar es Salaam

Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesaini makubaliano na Vyuo na Taasisi za Canada ya kutekeleza Mpango wa Uwezeshaji kupitia Ujuzi (ESP) wenye thamani ya takribani shilingi Bilioni 45.

Hayo yamesemwa Oktoba 26, 2023 Jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omari Kipanga wakati akimwakilisha Waziri Prof. Adolf Mkenda katika hafla ya makabidhiano ya Vifaa vya TEHAMA vya kufundishia na kujifunzia kutoka Serikali ya Canada vilivyotolewa kupitia Mradi wa ESP.

Swahili

Wizara ya Elimu Kuendelea Kukuza Tuzo za Waandishi Bunifu

Na WyEST
Dar es Salaam

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia katika bajeti ya Mwaka wa Fedha 2023/24 imepanga kuongeza nyanja za ushindani katika kuwania Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Prof. Carolyne Nombo Oktoba 24, 2023 Jijini Dar es Salaam alipomwakilisha Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda katika uzinduzi wa Kitabu cha Mwandishi Abdulrazak Gurnah kilichotafsiriwa katika lugha ya kiswahili kijulikanacho kwa jina la Peponi.

Swahili

Benki ya Dunia imeipongeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Benki ya Dunia imeipongeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kusimamia na kutekeleza Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) kwa ufanisi mkubwa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Oktoba 24, 2023  katika kikao cha pamoja cha kuanza kufanya tathimini ya utekelezaji wa  Mradi wa HEET kati ya Benki hiyo na Wizara, Kiongozi wa Timu ya Ufundi ya Benki ya Dunia Roberta Mallee Basset, amesema katika kipindi cha miezi sita iliyopita  inaonekana juhudi kubwa inayofanywa na wizara katika kusimamia utekelezaji wa mradi huo.

Swahili

Wataalam wa Manunuzi wa Mradi wa HEET wa Wakutana na Timu ya Benki ya Dunia

Timu ya Wataalam kutoka Benki ya Dunia imekutana na wataalam wa manunuzi kutoka Taasisi zinazotekeleza Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET)

Timu hiyo imekutana na wataalamu hao Oktoba 24, 2023 Jijini Dar es Salaam kujadili maendeleo ya manunuzi yanayohusu mradi huo na kujadili changamoto zinazojitokeza kwa lengo la kutafuta utatuzi wa pamoja

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS