WAZIRI MKUU BUNGENI
Mabadiliko yaliyofanyika kwenye Sera ya Elimu yamelenga maslahi mapana ya Taifa - Mhe. Kassim Majaliwa.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema mabadiliko yaliyofanyika kwenye Sera ya Elimu yamelenga maslahi mapana ya Taifa hivyo jamii inapaswa kupata uelewa wa kutosha juu ya umuhimu wa mabadiliko hayo.
Mhe. Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Bungeni jijini Dodoma wakati akieleza kuhusu kuidhinishwa kwa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023 na mitaala ya Elimu ngazi ya Elimu ya Awali, Msingi Sekondari na Elimu ya Ualimu.
Ujenzi wa jengo jipya ofisi za Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wafikia 80%
Ujenzi wa jengo jipya ofisi za Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wafikia 80%
UJENZI WA JENGO JIPYA OFISI ZA WIZARA YA ELIMU WAFIKIA 80%
#Prof. Nombo aridhishwa na maendeleo ya ujenzi, amtaka Mkandarasi kuongeza nguvukazi ili kukamilisha jengo kwa wakati.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo ameielekeza Kampuni ya China ya CRJE inayotekeleza mradi wa ujenzi wa majengo ya Wizara ya Elimu ya Sayansi na Teknolojia kuongeza nguvu kazi na muda wa kazi ili kuhakikisha jengo hilo linakabidhiwa ifikapo Disemba 15, 2023 kulingana na makubaliano ya mkataba.
Prof. Mkenda Azindua Ufadhili kwa wanafunzi wa kike wanaosoma Uhandisi Kwenye Sekta ya Usafirishaji
Vyuo na Taasisi Watakiwa Kuzingatia Viwango vya Ubora wa Elimu ya Ualimu Ngazi Zote Prof. Nombo
Prof. Mdoe Amtaka Mkandarasi wa Mradi wa EASTRIP DIT Mwanza kufidia Muda Uliopotea Kukamilisha kwa Wakati
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe Oktoba 29, 2023 amemtaka mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa mradi wa (EASTRIP) kuja na mpango kabambe wa kufidia muda uliopotea kwa ajili ya kukamilisha kwa wakati.
Prof. Mdoe amesema hayo alipotembelea Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Kampasi ya Mwanza kukagua maendeleo ya mradi wa kituo Cha Kikanda cha Umahiri wa Bidhaa za Ngozi (EASTRIP) na kukuta mradi ukiwa katika hali isiyoridhisha kuzingatia makubaliano ya mkataba na muda uliobaki kukamilisha mradi huo.
Prof. Adolf Mkenda ametembelea karakana mbalimbali katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ametembelea karakana mbalimbali katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji zinazotumika kufundishia na kujifunzia kwa vitendo
Prof. Mkenda amemtembelea Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amemtembelea kumsalimu Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania Sheikh Dkt Abubakar Zuberi Bin Ally nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.

