Prof Mkenda, UNICEF wajadili namna bora ya kutekeleza Sera ya Urejeshaji shuleni wanafunzi waliokatisha masomo

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda leo Novemba 8, 2023 Jijini Dodoma amekutana na kufanya mazungumzo na Timu ya Ujumbe wa UNICEF ukiongozwa na Mwakilishi wa Shirika hilo nchini Bi Eike Wisch.

Katika mazungumzo hayo viongozi hao wamejadili kuhusu Sera ya urudishwaji wa wanafunzi waliokatizwa masomo kutokana na sababu mbalimbali kama vile utoro, utovu wa nidhamu, kupata ujauzito na walioshindwa kuhudhuria masomo kwa muda mrefu.

Swahili

Prof. Nombo ahudhuria Mkutano Mkuu wa Mwaka wa UNESCO

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Carolyne Nombo ahudhuria Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) jijini Paris, Ufaransa.

Ameambata na Kamishna wa Elimu Nchini Dkt. Lyabwene Mtahabwa, Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO nchini Prof. Hamisi M. Malebo na Afisa Mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa Bi. Sekela Mwambegele.

Swahili

Prof. Nombo na Kamishna wa Elimu Dkt. Mtahabwa katika Ubalozi wa Tanzania Nchini Ufaransa

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo na Kamishna wa Elimu Dkt. Lyabwene Mtahabwa katika Ubalozi wa Tanzania Nchini Ufaransa ambapo wamekutana na Ndg. Amos Tengu Mkuu wa Utawala.

Prof. Nombo na ujumbe wake wako nchini Ufaransa kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS