Mhe. Kipanga akutana na Mkuu wa Wilaya ya Same

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omari Kipanga leo Nov 16, 2023 amefika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Same na Kukutana Mkuu wa Wilaya hiyo Kasilda Mgeni kabla ya kuelekea kwenye Kukagua maendeleo ya Shughuli za ujenzi wa VETA wilayani humo



Mhe. Kipanga yupo Mkoani Kilimanjaro kwa ziara ya kikazi kukagua utekelezaji na kufanya tathmini ya shughuli za ujenzi wa Vyuo vya VETA vya Wilaya katika Mkoa huo.

Swahili

Prof. Nombo amekutana na Balozi wa Ufaransa na Mwakilishi wa Kudumu wa UNESCO

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amekutana na Balozi wa Ufaransa na Mwakilishi wa Kudumu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Mhe. Philippe Franc wamezungumzia juu ya ufundishaji wa lugha ya Kifaransa katika mitaala ya Elimu Msingi na Ualimu pamoja na ufundishaji wa Kiswahili nchini Ufaransa.

Swahili

Prof. Nombo akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa na Mwakilishi wa Kudumu wa UNESCO

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa na Mwakilishi wa Kudumu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Mhe. Ali J. Mwadini wakifuatilia mkutano Mkuu wa Shirika hilo unaofanyika Paris nchini Ufaransa.

Swahili

Mradi wa HEET wakutanisha Sekta Binafsi, Viwanda na Taasisi za Elimu yaJuu.

 

Mradi wa HEET wakutanisha Sekta Binafsi, Viwanda na Taasisi za Elimu yaJuu kutafuta Muarobaini wa Ujuzi kwa Wahitimu  Na WyEST Dar es Salaam  Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) unaosimamiwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia umean

Na WyEST
Dar es Salaam

Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) unaosimamiwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia umeanzisha ushirikiano kati ya Taasisi za Elimu ya Juu, Sekta Binafsi na Viwanda ili kusaidia upatikanaji wa wahitimu wenye ubora na wenye kuhitajika katika soko la ajira.

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS