Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Romania wakishuhudia utiaji saini wa Mikataba mbalimbali ya ushirikiano

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mgeni wake Rais wa Romania Mhe. Klaus Iohannis wakati wakishuhudia utiaji saini wa Mikataba mbalimbali ya ushirikiano baina ya nchi hizo iliyotiwa saini na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) Prof. Raphael T. Chibunda na Waziri wa nchi wa masuala ya Dunia na Mikakati ya Kidiplomasia wa Romania Mhe. Traian- Laurentiu Hristea kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 17 Novemba 2023.

Swahili

Mhe. Kipanga amewataka Wasimamizi Ujenzi wa Chuo cha VETA Mwanga kuongeza idadi ya mafundi

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omari Kipanga amewataka wahandisi wanaosimamia ujenzi wa Chuo cha VETA cha Wilaya ya Mwanga kuongeza idadi ya mafundi ili kuharakisha ujenzi wa VETA hiyo ya Wilaya na kuongeza kuwa uwepo wa nguvu kazi ya kutosha kutafanikisha ujenzi kukamilika kulingana na ratiba.

Ametoa agizo hilo Novemba 16, 2023 wilayani Mwanga, Mkoani Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya ukaguzi na ufuatiliaji wa hatua za ujenzi wa Chuo hicho.

Swahili

Ongezeni Kasi na Umakini Ujenzi VETA Same- Mhe. Kipanga

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omari Kipanga amewataka wasimamizi wa Ujenzi wa Chuo cha VETA cha Wilaya ya Same kuongeza umakini na kasi ya ujenzi ili mradi huo ukamilike kwa wakati na kwa ubora.

Ameyasema hayo leo Novemba 16, 2023 alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi ikiwa pamoja na kutatua changamoto ambapo amesema lengo la kuhakikisha ifikapo mwezi wa 10 mwaka 2024 ujenzi uwe umekamilika.

Swahili

Mradi wa Shule Bora watoa Magari Elimu

#Ni katika kuimarisha kazi ya usimamizi na ufuatiliaji

Uwepo wa vitendea kazi ikiwemo magari ni muhimu katika kuwezesha kutekeleza kazi za kuimarisha utoaji elimu bora Nchini.

Leo tarehe 16, Novemba 2023, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Dkt. Franklin Rwezimula amepokea magari mawili yaliyotolewa kupitia mradi wa "Shule Bora" unaofadhiliwa na UK Aid.

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS