Menejimenti ya Wizara ya Elimu ikiongozwa na Prof. Mkenda Imekutana na Wadau wa Maendeleo wanaochangia katika Sekta ya Elimu nchini

Menejimenti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ikiongozwa Waziri Prof. Adolf Mkenda imekutana na kuwa na kikao cha pamoja Wadau wa Maendeleo wanaochangia katika Sekta ya Elimu nchini kutoka Balozi na Taasisi mbalimbali za Kimataifa.

Katika kikao hicho wadau wamepongeza juhudi za Serikali katika kuongeza uwekezaji katika elimu na kwa kusimamia vema utekelezaji wa Mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo na Mabadiliko ya Mitaala.

Swahili

Vitabu vya Kiada vya Milioni 86 Vyatolewa kwa Skuli Zanzibar

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania tarehe 22 Novemba, 2023 imekabidhi vitabu vya Kiada vyenye thamani ya shilingi 86,877,000 vya masomo mbalimbali kwa Skuli za Sekondari Zanzibar.

Vitabu hivyo vya kuanzia kidato cha I-VI vimetolewa kwa Skuli 6 za Sekondari za Mtende, Makunduchi, Kusini, Kizimkazi Mkunguni, Kizimkazi Dimbani na Hasnu Makame.

Swahili

Prof. Mkenda azindua kitabu kilichoandikwa na Prof. Joseph Kuzilwa

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda azindua kitabu kilichoandikwa na Prof. Joseph Kuzilwa ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe.

Prof. Kuzilwa amesema kitabu hicho chenye jina Usimamizi wa Mabadiliko Makubwa katika Taasisi za Elimu ya Juu, kina maudhui yanayohusu mabadiliko ya kihistoria ya Chuo hicho yaliyotokea tangu mwaka 1953 kilipoanzishwa kikiwa Kituo cha Mafunzo ya serikali za Mitaa mpaka kuwa Chuo Kikuu cha Mzumbe.

Swahili

Mabaraza ya Wahitimu ni Chachu ya Maendeleo Vyuo Vikuu - Prof. Mkenda

Waziri wa Elimu, Sayansi na teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema serikali inatambua umuhimu wa Mabaraza ya Wahitimu na Jumuiya mbalimbali katika Vyuo Vikuu, katika kuchangia Maendeleo ya miradi mbalimbali katika Vyuo husika.

Prof. Mkenda ametoa kauli hiyo Novemba 22, 2023 mjini Morogoro wakati akihutubia Baraza la Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe ambapo amesema serikali inajivunia michango ya Wajumbe wa Baraza hilo, ikiwemo mchango wa ujenzi wa mabweni kwa ajili ya Wanafunzi Ndaki ya Mbeya.

Swahili

Prof. Mkenda akiwa na rais wa Baraza la Wahitimu Chuo Kikuu Mzumbe

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akiwa pamoja na rais wa Baraza la Wahitimu katika Chuo Kikuu cha Mzumbe CPA. Ludovick Utouh wakati akikabidhiwa zawadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe.

CPA. Utouh amesema kwamba wanatambua mchango mkubwa wa Mhe. Samia katika kuinua kiwango cha Elimu nchini.

Swahili

Watafiti Vyuo Vikuu watakiwa kutatua changamoto katika Jamii

Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu Sayans i na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amewataka watafiti katika Vyuo Vikuu nchini kutambua kuwa wanawajibu wa kutatua changamoto zilizopo katika jamii.

Katibu Mkuu amesema hayo wakati akifungua zoezi la utoaji wa zawadi kwa Wanachuo, Watafiti na Viongozi wa Chuo waliofanya vizuri kwenye masomo katika Ndaki mbalimbali za Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS