Prof. Adolf Mkenda akiwa kwenye picha ya pamoja na Mawaziri waliowahi Kuhudumu katika WyEST

Prof. Adolf Mkenda akiwa kwenye picha ya pamoja na Mawaziri waliowahi Kuhudumu katika Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako, Dkt. Shukuru Kawambwa na Magreth Sitta wakati wa Maadhimisho ya Kilele cha Miaka 50 ya Baraza la Mitihani Tanzania yanayofanyika Jijini Dar es Salaam leo Disemba 16, 2023.

Swahili

Prof. Carolyne Nombo akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu waliowahi Kuhudumu katika WyEST

Prof. Carolyne Nombo akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu waliowahi Kuhudumu katika Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapi, Prof. Eliamani Sedoyeka, Dkt. Michael Francis na Prof. Hamis Dihenga wakati wa Maadhimisho ya Kilele cha Miaka 50 ya Baraza la Mitihani Tanzania yanayofanyika jijini Dar es Salaam leo Disemba 16, 2023.

Swahili

Baadhi ya Viongozi wa Serikali katika ofisi za Baraza la Mitahani Tanzania

Baadhi ya Viongozi wa Serikali, Wabunge, viongozi wa vyama vya siasa na wageni waalikwa wameshawasili katika ofisi za Baraza la Mitahani Tanzania tayari kushuhudia kilele cha Maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza hilo.



Mgeni Rasmi wa Maadhimisho hayo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hasaan ambaye anatarajiwa kuwasili wakati wowote kuanzia sasa.

Swahili

Prof. Carolyne Nombo apokea taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa HEET

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo leo Disemba 13, 2023 amepokea taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa Elimu Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) kutoka kwa wasimamizi wa mradi huo.

Katibu Mkuu huyo amewaelekeza wasimamizi hao kuhakikisha mradi unatekelezwa kwa ufanisi na wakati ili kufikia malengo yaliyowekwa. Aidha amehiza Wizara naTaasisi watekelezaji mradi kuongeza nguvu ya kutangaza kazi na mafanikio ya mradi huo.

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS