Wanafunzi 2,177 Wapangiwa Mikopo kwa Rufaa 2023/2024

Jumla ya Wanafunzi 2,177 waliopangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 7.26 bilioni baada ya kuwasilisha maombi ya rufaa kwa mwaka wa masomo 2023/2024 kwa kujaza taarifa na kuwasilisha nyaraka za kuthibitisha uhitaji wao.

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inawashauri Wanafunzi hao kuingia kwenye Akaunti za Kudumu za taarifa za mikopo maarufu (SIPA) ili kupata taarifa za kina kuhusu mikopo yao.

Swahili

WyEST inajivunia mchango wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) katika Sekta ya elimu

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inajivunia mchango wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) katika Sekta ya elimu.

Tunapoadhimisha miaka 50 ya Baraza hilo tunaendelea kukupatia elimu kuelekea utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2023 Toleo la 2023 na mabadiliko ya Mitaala ya elimu.

Pamoja na masuala mengine yanayohusu Elimu karibu Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam tuzungumze.

Swahili

Prof. Mkenda akimkabidhi Mshindi wa Jumla wa Tuzo za Uandishi wa Habari za Sayansi na Teknolojia upande wa kilimo

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akimkabidhi Mshindi wa Jumla wa Tuzo za Uandishi wa Habari za Sayansi na Teknolojia upande wa kilimo Tinsae Sinabe kutoka Shirika la Utangazaji la Ethiopia (EBC).

Mshindi huyo amepatiwa zawadi ya cheti cha Ushindi na hundi Dola za Marekani 3,500

Swahili

Uwajibikaji katika Uandishi wa Habari Unasaidia kuleta Mapinduzi katika Kilimo na Kulinda Usalama wa Chakula

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema serikali inatambua mchango wa Wanahabari unaosaidia kutangaza teknolojia zinazochangia katika mabadiliko endelevu ya Kilimo Barani Afrika.

Prof. Mkenda ametoa kauli hiyo Disemba 2, 2023 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza kwenye halfa ya Tuzo za Uandishi wa Habari za Sayansi na Teknolojia upande wa Kilimo yaani _OMAS Media Awards

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS