Prof. Mkenda ameshiriki mazungumzo yaliyoongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa GPE Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda leo Disemba 2023 jijini Dar es Salaam ameshiriki mazungumzo yaliyoongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE) Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa GPE Laura Frigenti.

