Prof. Nombo amekutana na Uongozi wa TAHLISO jijini Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Caloryne Nombo leo amekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) jijini Dodoma.

Kwa upande wake rais wa Shirika hilo Maria Thomas ameishukuru wizara ya Elimu kwa jitihada mbalimbali inayoendelea kufanya kuboresha elimu nchini na kuongeza fursa za upatikanji wake ikiwemo kujenga Kampasi za Vyuo Vikuu katika Mikoa mbalimbali.

Swahili

Ufaulu wa Upimaji wa Kitaifa Kidato cha Nne, Darasa la Nne Waongezeka.

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) leo Januari 07, 2024 limetangaza matokeo ya Mtihani Upimaji wa Kitaifa Kidato cha Pili, ambapo Jumla ya Wanafunzi 592,741 kati ya 694,769 wamefaulu sawa na asilimia 85.31. Kiwango hicho cha ufaulu kimeongezeka kwa asilimia 0.13 ikilinganishwa na asilimia 85.18 ya Wanafunzi waliofaulu Mtihani huo mwaka jana.

Akitangaza matokeo hayo Katibu Mtendaji wa NECTA Dkt. Said Mohamed amesema Jumla ya Wanafunzi 759,799 walisajiliwa kufanya Mtihani huo, wakiwemo Wasichana 405,878 na wavulana 353,921

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS