Serikali Kuboresha Maktaba 22 Nchini

**Bilioni 2 zatengwa kutekeleza kazi hii*

*Taasisi Binafsi yajenga Maktaba Ugweno.*

Serikali imetenga takriban Shilingi Bilioni 2 kwa ajili ya kuboresha Maktaba 22 ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa kuboresha Maktaba zote nchini ili kutoa fursa kwa wanafunzi, walimu na wakazi wengine wa ndani na wanaoishi nje ya nchi kupata maarifa.

Swahili

Prof. Mdoe Asisitiza Weledi katika Kusimamia Utekelezaji Mitaala Iliyoboreshwa

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe ametoa wito kwa Makatibu Tawala Wasaidizi Elimu na Maafisa Elimu wa Halmashauri Msingi kwenda kusimamia kwa weledi utekelezaji wa mitaala iliyoboreshwa ili iweze kuleta tija kwa mwanafunzi kama ilivyokusudiwa na Serikali.

Prof. Mdoe ametoa wito huo leo Januari 3, 2024 wakati akifungua Mafunzo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi Elimu pamoja na Maafisa Elimu wa Wilaya yaliyofanyika katika ukumbi wa shule ya Msingi Bernard Bendel Kola B Morogoro.

Swahili

Walimu ndio Elimu, Tuwasikilize ili Kuzijua Changamoto Zao - Dkt. Mtahabwa

Kamishna wa Elimu Tanzania Dkt. Lyabwene Mtahabwa ametoa wito kwa Wathibiti ubora wa shule na maafisa elimu kata kuwaheshimu walimu na kuwasikiliza ili kufahamu Changamoto zao hali itayosaidia kuboresha Sekta ya elimu nchini.

Dkt. Mtahabwa ametoa wito huo leo Desemba 30, 2023 Mkoani Morogoro wakati akifungua mafunzo ya mtaala ulioboreshwa kwa wathibiti ubora wa shule na maafisa elimu kata, mtaala unaotarajia kuanza kutekelezwa kuanzia Januari 2024.

Swahili

Dkt. Biteko ampongeza Prof. Mkenda mafanikio ‘Rombo Marathon and Ndafu Festival’

Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt. Dotto Biteko amewataka wakazi wa Rombo kuendelea kumpa ushirikiano Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda.

Dkt. Biteko ametoa wito huo hii leo wakati akifunga mashindano ya mbio ndefu ya Rombo na Uchomaji nyama ya Mbuzi yaani 'Rombo Marathon and Ndafu Festival’ yaliyofanyika hii leo katika eneo la msitu la Rongai,Tarakea wilayani Rombo.

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS