Taifa Linahitaji Wahitimu Mahiri na Waadilifu- Waziri Mkenda

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ameitaka jamii kushiriki katika kudhibiti vitendo vya udanganyifu katika vipindi vya mitihani, ili kulinda heshima ya elimu na Taifa kwa ujumla.

Prof. Mkenda ametoa rai hiyo leo Novemba 30, 2023 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza katika Ufunguzi wa Maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) ambapo amesema wizi wa mitihani unaharibu maadili ya watoto na heshima ya taifa.

Swahili

Tunapiga Vita na Kulaani Wizi wa Mitihani - Prof Mkenda

Tunapiga vita na kulaani wizi wa Mitihani, naomba tushirikiane kwa pamoja kuhakikisha tunadumisha uadilifu, uaminifu kulijenga Taifa letu kwa kupata Wahitimu mahiri.

Ni kauli yake Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akizungumza leo Novemba 30, 2023 jijini Dar es Salaam katika Ufunguzi wa Maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).

Swahili

Serikali Inaendelea Kuboresha Miundombinu ya Elimu na kuweka mazingira rafiki ya kujifunzia - Prof. Mkenda

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema Serikali inaendelea kuboresha miundombinu mbalimbali ikiwemo madarasa, kuweka vifaa, tunataka kuhakikisha uwepo wa mazingira rafiki ya watoto ya wa Kitanzania kupata Elimu bila kikwazo.



Waziri Mkenda ametoa kauli hiyo Novemba 30, 2023 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza katika sherehe za Ufunguzi wa Maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA)

Swahili

Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limejiandaa kutekeleza mabadiliko yanayotokana na Sera Mpya ya elimu - Dkt. Said Mohamed

Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limejiandaa kutekeleza mabadiliko yanayotokana na Sera Mpya ya elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 Toleo la 2023 na mabadiliko ya mitaala ya elimu, na kwamba rasimu ya awali ya maeneo yote ambavyo yanatakiwa kutekelezwa katika Sera hiyo tayari imeandaliwa.

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS