Wizara 5 Kujadiliana Mwarobaini Upungufu wa Wataaluma Vyuo vya Afya

Na WyEST
Dodoma

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknojia, Wizara ya Fedha, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Uwekezaji wakutana pamoja kujadili namna ya kutatua changamoto ya upungufu wa Wanataaluma katika Vyuo Vikuu na Kati vinavyotoa Elimu ya Afya na Tiba nchini.

Kikao hicho kilichofanyika Januari 23, 2024 Jijini Dodoma kimeongozwa na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe pia kimejadili changamoto ya miundombinu na vifaa vya kufundishia na kujifunzia katika vyuo hivyo.

Swahili

Prof Adolf Mkenda amepongeza kazi inayofanywa na Taasisi ya Mama ongea na Mwanao katika kusaidia wanafunzi wahitaji kupata vifaa

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda amepongeza kazi inayofanywa na Taasisi ya Mama ongea na Mwanao katika kusaidia wanafunzi wahitaji kupata vifaa vinavyowawezesha kupata elimu.

Ametoa kauli hiyo tarehe 23 Januari 2024 Katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam alipotembelewa na Kiongozi wa Taasisi hiyo Steven Mengele maarufu Steve Nyerere.

Swahili

Prof. Adolf Mkenda, amekutana Katibu Mkuu Taifa wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda, amekutana Katibu Mkuu Taifa wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi Bw. Gilbert Kalima, Jijini Dodoma.



Mkutano huo ulioshirikisha baadhi ya Viongozi wa Wizara ulilenga kujadili namna ya kushirikiana katika kuboresha shule zilizo chini ya Jumuiya hiyo.

Swahili

Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Elimu imeitaka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kujitangaza kuwezesha vijana kujinga ili kupata mafunzo

Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Elimu, Utamaduni na Michezo imeitaka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kujitangaza kuwezesha vijana kujinga ili kupata mafunzo mbalimbali yanayotolewa.

Akizungumza Januari 20,2024 wakati wa ziara ya Kamati hiyo katika Ofisi za Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam Kaimu Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Musa Siima amesema Taasisi ya Watu Wazima inafanya kazi nzuri ya kutoa elimu kwa njia mbadala kwa vijana walio nje ya mfumo rasmi ambayo inawasaidia vijana kutimiza ndoto zao za elimu.

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS