Prof. Mkenda ameiambia Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Elimu kuwa watoto wote waliotoka nje ya mfumo rasmi wa elimu kwa sababu zozote zile wanarudi shule
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ameiambia Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Elimu, Utamaduni na Michezo kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha watoto wote waliotoka nje ya mfumo rasmi wa elimu kwa sababu zozote zile wanarudi shule ili kupata elimu na ujuzi na kutimiza ndoto zao za kuwaletea maendeleo binafsi na ya Taifa.






