Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu imekutana na Wizara ya Elimu kujadili utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya Elimu

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imekutana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na kujadili utekelezaji wa majukumu ya Elimu ya Ualimu na maendeleo ya elimu ya ufundi na mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) ambapo kamati hiyo imeridhishwa na utekelezaji na mipango ya kuimarisha ngazi hizo za Elimu.

Swahili

Shule ya Sekondari yenye Miundombinu ya Kisasa Kuzinduliwa hivi Karibuni

#Ujenzi wafikia 96%

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Dodoma City inayojengwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia maarufu kama Shule ya Mfano, Jijini. Dodoma.

Akizungumza Januari 09, 2024 baada ya kukagua ujenzi huo, Prof. Mkenda amesema kwa hatua iliyofikia na kwamba Wizara iko tayari kwa uzinduzi kabla yavkuikabidhi Ofisi ya Rais Tamisemi.

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS