Walimu ni Nguzo ya Elimu Nchini - Prof. Nombo

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amewataka Wakufunzi katika Chuo cha Ualimu tarajali Korogwe jijini Tanga kufahamu mwelekeo wa elimu, na kuhakikisha wanawajibika kikamilifu katika kutekeleza mabadiliko ya Elimu yanayolenga kuimarisha ufundishaji kidijitali.



Nombo ametoa rai hiyo Mei 29, 1024 jijini Tanga wakati akizungumza na Wakufunzi na Wafanyakazi Mwega wa Chuo hicho kuhusu masuala mbalimbali ya Elimu.

Swahili

Prof. Carolyne Nombo akiwa Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe kuona maendeleo ya utoaji Elimu

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo akiwa Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe kuona maendeleo ya utoaji Elimu na utekelezaji wa Mitaala iliyoboreshwa.



Shule hiyo kongwe iliyoanza Mwaka 1965 ni miongoni mwa Shule zinazotoa Mafunzo ya Amali, ina mchepuo wa Kilimo, Ushoni na Mapishi.

Swahili

Prof. Carolyne Nombo yupo katika Wilaya ya Korogwe, katika ziara Chuo cha Ualimu Korogwe na Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo yupo katika Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga katika ziara Chuo cha Ualimu Korogwe na Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe.

Swahili

Ni Heshima kubwa kwa Mkoa wetukuwa Mwenyeji wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu - Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian amesema ni heshima kubwa kwa mkoa huo kuwa Mwenyeji wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu, Wanatanga nawakaribisha kutembelea Maonesho kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo Teknolojia.

Swahili

Maonyesho ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yameibua fursa mbalimbali kwa Wananchi katika kujifunza Teknolojia mbalimbali za kisasa.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amesema Monyesho ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yameibua fursa mbalimbali kwa Wananchi, Wadau mbalimbali wa Maendeleo pamoja na Vijana katika kujifunza teknolojia mbalimbali za kisasa.

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS